Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 20:35

Wakuu wa ulinzi wa Korea Kusini, Japan na Marekani wanafanya operesheni ya pamoja


Mawaziri wa ulinzi wa Korea Kusini, Japan na Marekani wamekubaliana kuanza operesheni ya kushirikiana kuhusu makombora ya Korea kaskazini
Mawaziri wa ulinzi wa Korea Kusini, Japan na Marekani wamekubaliana kuanza operesheni ya kushirikiana kuhusu makombora ya Korea kaskazini

Mawaziri hao walijadili kuimarisha ushirikiano wao wa pande tatu, wakati wakikabiliana na mazingira magumu ya usalama, Kihara aliwaambia waandishi wa habari. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mawaziri hao watatu kufanya mkutano kama huo, alisema.

Wakuu wa ulinzi kutoka Korea Kusini, Japan na Marekani wamekubaliana mwezi Disemba kuanza operesheni ya kushirikiana takwimu halisi kuhusu makombora ya Korea Kaskazini, wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema Jumapili.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, alikutana na mwenzake wa Korea Kusini Shin Won-sik mjini Seoul leo Jumapili na waziri wa ulinzi wa Japan Minoru Kihara, alijiunga katika mkutano huo kwa njia ya mtandao.

Mawaziri hao walijadili kuimarisha ushirikiano wao wa pande tatu, wakati wakikabiliana na mazingira magumu ya usalama, Kihara aliwaambia waandishi wa habari. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mawaziri hao watatu kufanya mkutano kama huo, alisema. “Tunathibitisha kwamba tunafanya marekebisho kwa kasi, na kuleta mchakato huo katika hatua ya mwisho”, Kihara aliongeza.

Rais wa Marekani Joe Biden alikubaliana na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida katika mkutano wa Agosti 18, kwamba kufikia mwishoni wa mwaka huu nchi hizo tatu zitashirikiana takwimu za onyo la makombora ya Korea Kaskazini katika muda halisi.

Forum

XS
SM
MD
LG