Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:39

Macho yote sasa New Hampshire katika uchaguzi wa awali


Mgombea kiti wa chama cha Democratic Seneta Bernie Sanders Des Moines, Iowa.
Mgombea kiti wa chama cha Democratic Seneta Bernie Sanders Des Moines, Iowa.

Wagombea urais wa Marekani hivi sasa wanalenga juhudi zao kwenye jimbo la New Hampshire.

Huku wagombea urais wa Marekani hivi sasa wakilenga juhudi zao kwenye jimbo la kaskazini-mashariki la New Hampshire, kwa mara nyingine tena wataingia kwenye duru ya midahalo kuelezea azma zao kabla ya wapiga kura kufanya maamuzi siku ya Jumanne.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, akiwa na ushindi mdogo kutoka jimbo la Iowa, anashiriki kwenye mkutano unaowakutanisha wapiga kura Jumatano usiku na Seneta Bernie Sanders. Warepublican wamepanga kufanya mdahalo wao siku ya jumamosi.

XS
SM
MD
LG