Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 08:58

Wafuatiliaji wa kimataifa watua Tanzania

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Tanzania

Akizungumza na Sauti ya Amerika Emanuel Kawishe mkurugenzi wa idara ya huduma za kisheria katika Tume ya uchaguzi ya Tanzania, pia amesema vyama vya kisiasa vimekamilisha masharti yote kisheria ili kuwaruhusu kufanya kampeni na kushiriki katika kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi mkuu.

Ofisa mwenye cheo cha juu wa tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania amesema zaidi ya wafuatiliaji 140 wa kimataifa wameshaingia nchini humo kufuatilia uchaguzi wa urais na bunge.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Emanuel Kawishe mkurugenzi wa idara ya huduma za kisheria katika Tume ya uchaguzi ya Tanzania, pia amesema vyama vya kisiasa vimekamilisha masharti yote kisheria ili kuwaruhusu kufanya kampeni na kushiriki katika kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi mkuu.

Tanzania ina vyama 22 vilivyosajiliwa .Maelezo yake yamekuja baada ya maafisa wa tume ya uchaguzi kutoa maelezo kwa wawakilishi wa makundi ya kufuatilia uchaguzi katika mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam.

Amesema mkutano huo ni sehemu ya ahadi ya tume ya uchaguzi kuhakikisha kuwa inakuwa na ushirikliano bora na waangalizi wa kimataifa wakati wakijiandaa kufanya kazi ya kufuatilia uchaguzi. Kawishe amesema tume ya uchaguzi inajiandaa kutangaza matokeo siku hiyo hiyo mara upigaji kura utakapomalizika.

XS
SM
MD
LG