Upatikanaji viungo

Wafadhili wa kimataifa wameahidi kutowa msaada wa dola milioni 300 ili kuisaidia Somalia baada ya kuitikia wito wa kusaidia nchi hiyo kuimarisha vyombo vyake vya usalama, mahakama na fedha.

Katika mkutano wa viongozi mjini London siku ya Jumanne, ulotayarishwa kwa pamoja na Rais Hassan Sheikh Mohamed na Waziri Mkuu wa uingereza David Cameroon wajumbe walihimizwa kusaidia kuimarisha uwezo wa serikali ya Mogadishu.

Akizungumza na Sauti ya Amerika baada ya mkutano, mjumbe maalum wa Umoja wa Matiafa kwa Somalia Balozi Augustine Mahiga, anasema wameridhika na matokeo ya mkutano kwani wafadhili wameweza kuridhika na kazi za serikali mpya na kwamba Somalia hivi sasa imepiga hatua kubwa katika kurudisha uthabati.

Balozi Mahiga anasema viongozi walizungumzia kwa urefu pia mchango wa Afrika katika usalama wa Somalia na nchi jirani, "ni lazima kwa jeshi la Africa liongezewe uwezo wake, hasa uwezo wa kuwafuatilia Al-Shabab katika maeneo ya mashambani"

Mwandishi wa idhaa ya Kisomali ya Sauti ya Amerika, Daud Weso anasema mkutano huo ni muhimu katika kuwahahikishia wasomali kwamba dunia iko pamoja nao na kwamba wanabidi kuchukua hatua kubwa kuimarisha usalama na hasa matumizi ya fedha.

Maoni yako

Onyesha maoni

XS
SM
MD
LG