Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 15:51

Wabunge wanawake wa Somalia wakutana


Wanawake wa Somalia mjini Mogadishu
Kuna usemi kuwa “Ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima”. Hii ndio sababu wabunge wanawake kutoka Somalia wanakutana mjini Kampala kujadili shida zinazowakumba. Lengo lao likiwa kuhakikisha wanawake wanajumwishwa kikamilifu kwenye maamuzi na utungaji wa sheria za Somalia kwa sababu kina mama wanazielewa shida zinazoikumba jamii na njia bora za kuzitatua .

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:55 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Somalia iliunda serikali mpya mwezi wa nane mwaka 2012 miaka 21 baada ya kukosa uongozi mwafaka wa kisiasa kufuatia kung'olewa mamlakani rais Siad Barre mwaka wa 1991.Wanajeshi mbali mbali kutoka mashariki mwa Afrika chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika Amisom kuanzia mwaka wa 2007 walikwenda Somalia kuisaidia serikali ya mpito kudumisha amani.

AMISOM iliweza kuyakomboa maeneo kadhaa ya Somalia kutoka mikononi mwa waasi wa Al-shabaab na hatimaye mwezi wa nane Agosti 2012, Somalia ikaunda serikali na bunge mpya. Bunge lililoundwa lina wabunge 275.

Ingawa wanawake waling'ang'ana ili angalau wapate asilimia thelatini ya uwakilishi bungeni, hilo halikufanyika. Walipata asili mia kumi na nne peke yake. Asili mia kumi na nne ikiwa ni wanawake 38. Ishirini na nane kati ya wanawake hawa sasa wako mjini Kampala kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa wabunge wa kike wa Somalia.

Wabunge wengine wa kike wanaoshiriki wanatoka Burundi, Djibouti, Kenya, Rwanda na Uganda. Nchi hizi zote isipokuwa Rwanda zina majeshi yake nchini Somalia kuisaidia serikali ya Somalia kudumisha amani.

Lydia Wanyotu kutoka Uganda ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mbunge wa bunge la Afrika mashariki anasema mkutano huu uliandaliwa na kitengo cha jinsia cha AMISOM. Naye naibu mkuu wa AMISOM Wafula Wamunyinyi anasema mojawapo ya juhudi zao ni kutekeleza jukumu walilopewa na baraza la Usalama la Umoja wa Afrika na kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa.

Hapo mwanzoni jukumu la AMISOM lilikuwa kuwalinda viongozi na taasisi za serikali pamoja na kusaidia kwenye mchakato wa mazungumzo na kuridhiana wakati wa serikali ya mpito. Pia walipewa jukumu la kutoa msaada wa kibinadamu na kuzijenga taasisi za serikali haswa zile za usalama na kuboresha utendaji kazi kwenye ofisi za serikali.

Mkutano huu ni mojawapo wa majukumu ya AMISOM kuhakikisha kuwa serikali mpya ambayo itaongoza Somalia kwa kipindi cha miaka minne ijayo inaleta amani ya kudumu na kujenga mazingira mazuri ambayo yatawawezesha wasomali wanaoishi ugenini kurudi Somalia ili kuijenga nchi yao.
XS
SM
MD
LG