Wabunge wa Marekani wanaangalia maelezo ya makubaliano ya kuongeza kiwango cha kukopa kwa Marekani kabla ya kura zinazotarajiwa katika siku zijazo wakati ambapo Rais Joe Biden na spika wa baraza la wawakilishi Kevin McCarthy wakiwasihi waidhinishe.
Pendekezo hilo ni pamoja na kuondoa ukomo wa deni lililopo la dola trilioni 31.4 hadi Januari 2025 na makubaliano ya bajeti ya miaka miwili ambayo yataweka matumizi ya serikali kuu katika mwaka wa fedha kuanzia Oktoba na kuongezeka kwa asilimia moja katika miezi 12 ijayo hadi mwaka 2025.
Sehemu nyingine za makubaliano hayo ni kupunguza kuajiri mawakala zaidi katika idara ya kukusanya kodi, jambo jingine ni kwa majimbo kurudisha dola bilioni 30 katika msaada wa janga la virusi vya corona kwa serikali kuu, na kuongeza umri kutoka miaka 50 hadi 54 kwa wale wanaohitajika kufanya kazi ili kupokea msaada wa chakula.
Biden na McCarthy walifikia makubaliano hayo Jumamosi jioni baada ya wiki kadhaa za mazungumzo.
Forum