Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 08:42

Wabunge wa Kenya wahitilafiana na Magavana juu ya utekelezai katiba


Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto wakiwa Mombasa wakati wa kampeni za uchaguzi Februari 2013
Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto wakiwa Mombasa wakati wa kampeni za uchaguzi Februari 2013
Karibu miaka miwili iliyopita wakati wakenya walipoidhinisha katiba mpya ya mageuzi ya mfumo wa utawala nchini mwao , kila mtu alisifu na kueleza kua ni moja wapo ya katiba nzuri kabisa barani Afrika.

Lakini mwaka mmoja baada ya mfumo mpya wa utawala wa Ugatuzi, kama inavyofahamika huko Kenya kuchukua madaraka, maoni yamegawika kabisa. Kuna baadhi wanaoeleza kwamba kinachotokea hii leo ni upimaji nguvu na kujenga ushawishi na ngome za makundi ya kisiasa.

Hata hivyo kuna wengine ambao huwenda wakawa wengi wanasema kuna matatizo msini katika sheria na inabidi kufanyiwa marekebisho baadhi hata wakipendekeza kupunguza County zilizopo na kufanya mageuzi ya kina ya kisheria.
please wait

No media source currently available

0:00 0:09:52 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mchambuzi wa masuala ya kisheria wakili Harun Ndumbi, anasema "mvutano uliyoko hivi sasa, ninaweza kuuita ni kiburi cha wanasiasa na sera zao. Kwa sababu wanasiasa ikiwa wale wabunge wa Bunge la Taifa au wale wa Mabunge ya County wamewafikiana kwamba ikihusu suala la kumondoa Gavana kwa utaratuibu wa kumfungulia mashtaka bungeni, 'impeachment', basi mahakama haina ruhusa kuingilia kati."

Changamoto kuu inayojitokeza hivi sasa ni nani mwenye mamlaka ya kusimamia utawala bora baina ya bunge na mahakama, ikiwa ni tatizo linalotokota kukiwa na magavana tiwsa walopata idhini kutoka mahakama kwamba hawana haja kwenda mbele ya Baraza la Senet , kujitetea kuhusiana na utumiaji mbaya wa fedha.

Mwishoni mwa wiki Rais Uhuru Kenyatta akiwa katika mkutano wa hdahra mjini Kericho alitoa wito kwa mahakama kuliachia bunge kufanya kazi. nae kiongozi wa upinzani wa muungano wa CORD Raila Odinga kujibu kwamba inabidi watu wote waheshimu maamuzi ya mahakama.

Bw. Ndumbi anasema wanasheria na wachambuzi wengi wanaamini maamuzi ya mahakama yanabidi kuhseshimiwa kwa vyevote vile kwani katiba inatoa nafasi ya mhakama kuwa huru na uwezio wa mtu kukata rufaa na kufikisha mashtaka yake hadi mahakama kuu.
XS
SM
MD
LG