Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 14:44

Waandishi watiwa kifungoni Sudan


Rais wa Sudan Omar al-Bashir

Mwanasheria wa waandishi watatu wa upinzani wa Sudan anasema wamekutwa na hatia ya kuandika taarifa za uongo na kuhukumiwa kwenda jela hadi miaka mitano.

Mwanasheria wa waandishi watatu wa upinzani wa Sudan anasema wamekutwa na hatia ya kuandika taarifa za uongo na kuhukumiwa kwenda jela hadi miaka mitano.

Wakili wa utetezi Abel Moneim Osma anasema atakata rufaa dhidi ya hukumu hizo. Hakukuwa na matamshi ya mara moja kutoka serikali ya Sudan.

Waandishi hao wanne walikuwa wakifanya kazi na gazeti lililofungiwa la Rai Al Shaab linalohusishwa na wapinzani wa kiislam wa Sudan.

Wakili huyo wa utetezi anasema walishitakiwa kwa kuandika ripoti za uongo kuhusu kiwanda kimoja huko Sudan kwamba kinatengeneza silaha kwa ajili ya Iran. Pia waliandika makala zikieleza kuwa rais Omar Al Bashir hana uungaji mkono mkubwa.

Wakili wao alisema Abu Zar al-Amin mhariri mkuu msaidizi wa gazeti hilo alihukumiwa miaka mitano jela wakati waandishi wengine wawili Ashraf Abdelazizi na Tahir Abu Jawhara kila mmoja alihukumiwa miaka miwili jela.

XS
SM
MD
LG