Waandamanaji wenye hasira walivamia ofisi za chama tawala cha Baath katika jimbo la kusini mwa Syria siku ya Jumatano wakati maandamano yakiongezeka dhidi ya serikali ya nchi hiyo wakati wa mgogoro mkubwa wa kiuchumi na kifedha ulioikumba nchi hiyo iliyokumbwa na vita.
Wanaharakati wa upinzani wamesema waandamanaji pia walifunga barabara kuu inayounganisha jimbo la Druze na Sweida kuelekea mji mkuu Damascus katika maandamano ya kuipinga serikali yaliyozuka Jumanne usiku. Maandamano hayo yalichochewa na hali mbaya ya maisha na mfumuko wa bei ambao uliongezeka baada ya uamuzi wa Rais Bashar al-Assad wiki iliyopita wa kuongeza maradufu mishahara ya sekta ya umma na malipo ya uzeeni.
Maandamano hadi sasa hayajasambaa kwenye ngome za serikali katika pwani ya Mediterania, mji mkuu Damascus na miji mikubwa ikiwemo Aleppo na Homs. Hata hivyo matukio hayo pia yamefanyika katika mkoa wa Daraa unaopakana na Jordan.
Uchumi wa eneo hilo umedorora na uhalifu umeongezeka tangu vikosi vya serikali walipokamamta tene eneo hilo mwaka 2018. Serikali ya Syria haijajibu lolote juu ya maandamano hayo.
Forum