Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:13

Waandamanaji wameandamana Morocco kupinga kupanda kwa gharama za maisha


Umati wa waandamanaji huko Morocco wakipinga kupanda kwa gharama za maisha
Umati wa waandamanaji huko Morocco wakipinga kupanda kwa gharama za maisha

Waandamanaji kutoka chama cha Democratic Labour Confederation (CDT) walikusanyika katika uwanja wa kihistoria wa Casablanca wakielezea kutoridhishwa na kupanda kwa bei pamoja na kupunguzwa uwezo wa ununuzi

Mamia ya watu waliandamana Jumapili katika mji mkuu wa kiuchumi wa Morocco, Casablanca kupinga kupanda kwa gharama za maisha katika taifa hilo la Afrika Kaskazini na kutaka hatua zichukuliwe na serikali, waandishi wa habari wa shirika la AFP wamesema.

Waandamanaji kutoka chama cha Democratic Labour Confederation (CDT) walikusanyika katika uwanja wa kihistoria wa Casablanca wakielezea kutoridhishwa na kupanda kwa bei pamoja na kupunguzwa uwezo wa ununuzi, mwandamanaji Abdellah Lagbouri ameliambia shirika la habari la AFP.

Lagbouri alikuja kwenye mkutano kutoka Agadir mji ulio kusini zaidi kwenye pwani ya Atlantiki. Waandamanaji wengine pia walisafiri kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hadi Casablanca kwa ajili ya maandamano hayo.

Waandishi wa AFP walishuhudia makabiliano kati ya maafisa wa usalama na waandamanaji lakini walisema maandamano hayo yalimalizika bila ya kutokea tukio kubwa.

Forum

XS
SM
MD
LG