Uchaguzi huo wa awali umepangwa na upinzani licha ya upinzani mkubwa pamoja na vizingiti kutoka kwa serikali ya Maduro. Zoezi hilo linaonekana kuwa la kidemokrasia kwa kuwa upinzani uliyogawanyika umeshirikiana kupatia taifa hilo la Kusini mwa Amerika nafasi ya kufanya uchaguzi wa rais tangu 2012.
Hata hivyo matokeo yake yatategemea ushirikiano wa serikali ya Maduro. Ingawa utawala huo mapema wiki iliyopita uliruhusu upinzani kuchagua magombea wao kwenye uchaguzi wa rais mwaka ujao, ulizuia Maria Corina Machado mwenye umaarufu mkubwa kushiriki kwenye zoezi hilo.
Machado ambaye alikuwa mbunge anayeunga mkono utawala wa sera ya soko huru, amekuwa mpinzani mkubwa wa utawala wa chama cha Maduro cha United Socialist Party of Venezuela.
Forum