Umoja wa Mataifa umesema umefikia makubaliano na serikali ya Syria juu ya kupeleka misaada katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi kutoka Uturuki, na kuzusha wasiwasi miongoni mwa makundi ya misaada ambayo yaliitaka Damascus isihusishwe.
Chini ya makubaliano ya mwaka 2014, misaada mingi ya kimataifa ilipitia katika njia ya Bab al-Hawa kutoka Uturuki bila idhini ya Damascus. Lakini mwezi uliopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilishindwa kufikia muafaka juu ya kuongeza muda wa utaratibu huo na Umoja wa Mataifa ulisema pendekezo la Syria la kuiweka wazi njia hiyo kwa miezi mingine sita lina masharti yasiyokubalika.
Jumanne jioni msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema Katibu Mkuu anakaribisha maelewano yaliofikiwa Jumatatu na Umoja wa Mataifa na serikali ya Syria juu ya kuendelea kutumika kwa kivuko cha mpakani cha Bab al Hawa kwa muda wa miezi sita ijayo.
Forum