Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:12

Umoja wa Mataifa kuongeza majeshi ya AMISOM


Kikosi cha Umoja wa Afrika Somalia (AMISOM)
Kikosi cha Umoja wa Afrika Somalia (AMISOM)
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeagiza nyongeza ya wanajeshi 4,000 zaidi kusaidia kikosi cha Umoja wa Afrika kinachopambana na wanamgambo wa Somalia.

Baraza hilo pia liliidhinisha Umoja wa Mataifa kutoa msaada wa chakula , maji na vifaa vingine kwa jeshi la kitaifa la Somalia wakati linapofanya operesheni za pamoja na kikosi cha Umoja wa Afrika nchini humo kinachojulikana kama AMISOM.

Uingereza ilidhamini azimio hilo kupitia balozi wake katika Umoja wa Mataifa, Mark Lyall Grant. Balozi huyo alisema kikosi cha AMISOM kimefanya juhudi kubwa kudhoofisha nguvu za kundi la wanamgambo wa al- Shabab nchini Somalia.
XS
SM
MD
LG