Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:09

Ujasiriamali DRC : Mwanamitindo anayetumia mabaki ya nguo


Mwanamtindo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Sagesse Kalendira, akiwa kazini, Goma
Mwanamtindo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Sagesse Kalendira, akiwa kazini, Goma

Mshonaji wa nguo mjini Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amejizolea umaarufu mkubwa kwa kushona nguo za mitindo ya kuvutia kwa kutumia mabaki ya vitambaa viliyvokatwa na mara nyingi hutupwa wakati wa ushonaji.

Sagesse Kalindera, ameanzisha chapa yake maarufu kwa jina Moda Kalisa.

Sagesse Kalindera ni msichana mwana mitindo wa miaka 23 katika mji wa Goma. Karakana yake imekuwa ikishona nguo za aina yoyote kwa kutumia vitenge. Kawaida kwa washonaji nguo mabaki ya nguo huchomwa na mengine kutupwa lakini amekuja na mtindo wakutumia mabaki ya vitenge kuwa vivutio sio tu ndani ya nyumba lakini pia ofisini.

‘Humu ndani tunashona nguo za aina zote na tukimaliza mabaki ya nguo tunayoyaita bitepe hatuyatupi tunayapa tena maisha kwa kutengeneza vitu vingine vya thamani ili viweze kutumika tena. tunatengeneza vitu mbalimbali vya kupamba nyumbani na ofisini,’ amesema Kalindera.

Tofauti na washonaji wengine

Katika karakana nyingi za ushonaji hapa nchini vitepe ambavyo ni ya vitenge hutupwa jalalani wengine wakivichoma na hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira lakini Sagesse anasema mradi wake pia unalenga kupambana na hali hiyo.

‘Tuliona kwamba watu wengine wanaoshona nguo wanatupa wengine wanazichoma. hivyo tuliona kwamba ule moshi unaharibu mazingira ndio maana tuliona tutumie njia za kusafisha mazingira.’

Hata hivyo sasa mabaki ya nguo yamekuwa ni biashara jambo ambalo linampa ugumu joelle.

‘Baada ya kuanzisha mradi huu na kukusanya mabaki ya nguo kwenye karakana za ushonaji sasa wenzetu walipoona tunakuja kuchukua kila siku sasa wameanza kuziuza.’

Baadhi ya nguo anazoshona mwanamitindo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Sagesse
Baadhi ya nguo anazoshona mwanamitindo wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Sagesse

Juhudi za kukuza vipaji vya vijana na kubuni ajira

Wataalami wa uchumi wanasema kwamba hatua ya ubunifu na kujiajiri ndio njia pekee ya kujikwamua hasa kwa vijana nchini DRC. Bwana Katembo Juma ameipongeza mradi wa AFIMA huku akiomba vijana wengine kuiga mfano huo.

‘Tunashukuru kwa sababu yeye amekuwa mfano mzuri kwetu kwasababu anajitegemea na lengo letu kama wajasiria mali wa Kivu ni kuwaleta vijana waweze kujitegemea. Tuna nchi ambayo ina fursa kubwa lakini vijana wengi wanakuwa wenye kukosa kazi. Ndio maana tunataka vijana waone hizo fursa ambazo Kalindera ameweza kuziona na kujaribu maana amekuwa mfano nzuri wa kuigwa tunafurahia na kutosheka,’ amesema Katembo Joel, mkurugenzi wa kundi la wajasiriamali mjini Goma.

Mbali na mchango wake katika mapambano dhidi ya uchafuzi wa mazingira, kupitia mpango wa modaKalisya, Sagesse Kalindera pia ametengeneza ajira kwa marafiki zake wengine wawili na hivyo kuwaruhusu kubadilika katika ushonaji, eneo ambalo wanalipenda sana.

Imetayarishwa na Byobe Malenga, VOA, Kinshasa

XS
SM
MD
LG