Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 02:16
VOA Direct Packages

Uholanzi kuweka masharti mapya katika upelekaji wa teknolojia, China kutokana na sababu za kiusalama


Picha za chip zinazotumika kwenye utengenezaji wa kompyuta

Serikali ya Uholanzi Jumatano imesema kwamba inapanga kuweka masharti mapya kwa upelekaji wa  teknolojia za computer nchini China, ili kulinda usalama wake wa taifa.

Uholanzi inaonekana kujiunga na Marekani ambayo ilitangaza hatua sawa na hiyo hapo awali. Oktoba mwaka jana Marekani iliweka kanuni mpya kwenye upelekaji wa vifaa vya kutengeneza chip za computer nchini China, lakini kwa hilo kufaulu, inahitaji ushirikiano wa mataifa kama Uholanzi na Japan ambayo pia hutengeneza vifaa hivyo.

Mataifa hayo washirika yamekuwa kwenye mazungumzo kushusu suala hilo kwa miezi kadhaa. Waziri wa biashara wa Uholazi Liesje Schreinemacher ametangaza uamuzi huo kupitia barua kwa bunge, akisema kwamba hatua hiyo itaanza kutekelezwa kabla ya msimu wa joto kuanza.

Barua yake haikutaja China moja kwa moja ambayo ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Uholanzi, wala kampuni ya ASML Holding NV, ambayo ni kubwa zaidi ya teknolojia barani Ulaya, na mshirika wa karibu wa mataifa yanayotengeneza vifaa vya semiconductor.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG