Wakosoaji wake wanasema kwamba matamshi hayo yanahujumu ushirikiano wa mataifa ya Atlantic, wakati ulimwengu ukishuhudia taharuki za kisiasa za kieneo. Macron aliitembelea Beijing Aprili 5-8 akiandamana na mkuu wa EU, Ursula von der Leyen, kwa sehemu moja kuisihi china kusaidia katika kumaliza uvamizi wa Russia wa Ukraine.
Miongoni mwa watu wangine walioandamana na viongozi hao ni wafanyabiashara mashuhuri kutoka Ulaya, na ambao walitia saini mikataba kadhaa ya kibiashara. Kufikia sasa, China haijakemea uvamizi wa Russia wa Ukraine ulioanza Februari mwaka jana, na rais Xi Jinping pia alijiepusha kuzungumzia hilo wakati wa ziara ya Macron.