Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alifanya mazungumzo na mwenzake wa Sri Lanka siku ya Jumamosi juu ya eneo la wazi na la umoja la Indo-Pacific katika ziara ya kwanza kama kiongozi wa Ufaransa katika taifa hilo la kisiwa cha Bahari ya Hindi.
Akiwa mkopeshaji wa nne mkubwa kwa Sri Lanka, Ufaransa iliahidi ushirikiano katika marekebisho ya muundo wa madeni ili kulisaidia taifa hilo kujikwamua kutoka kwenye mgogoro wake wa kiuchumi.
Macron aliwasili nchini Sri Lanka Ijumaa usiku kufuatia ziara yake katika eneo la South Pacific kuadhimisha miaka 75 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili, ofisi ya Rais wa Sri Lanka imesema.
Rais wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe alisifu jukumu muhimu la Ufaransa katika masuala ya kimataifa, hasa katika maeneo kama vile kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa, marekebisho ya deni la kimataifa, na masuala yanayohusiana na eneo la Indo-Pacific.
Forum