Ufaransa inapeleka vikosi 10,000 ili kuongeza usalama katika baadhi ya maeneo muhimu kufuatia shambulio baya la kigaidi la wiki iliyopita mjini Paris, Ufaransa.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, aliwaambia Wanahabari Jumatatu, kwamba vikosi vitakuwa tayari siku ya Jumanne.
Naye waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernad Cazeneuve amesema karibu nusu ya vikosi vitakuwa vinalinda shule 717 za kiyahudi.
Mawaziri hao walizungumza masuala hayo ya ulinzi katika kikao cha baraza la mawaziri na Rais wa Ufaransa, Francois Holande, kilichojadili hasa juhudi za ulinzi.
Pia siku ya Jumatatu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry atasafiri kwenda Ufaransa kwa mazungumzo ya kupambana na ghasia zinazotokana na msimamo mkali.
Bwana Kerry, pia ameongeza kwamba Marekani kwa kutumia vyombo vyake vya kijasusi, na idara ya upelelezi wa makosa ya jinai FBI inashirikiana na wenzao wa Ufaransa.