Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:05

Mahakama ya Austria yafuta matokeo ya uchaguzi


Mahakama kuu ya Austria imeamua leo kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi Mei, baada ya kesi iliyowasilishwa na mmoja wa wagombea, NORBERT HOFER, ambaye alishindwa kwa kura chache kwenye uchaguzi huo.

Katika uamuzi wake, Jaji GERHARD HOLZINGER, ambaye ndiye mkuu wa mahakama ya katiba nchini humo, amesema kuwa hoja iliyowasilishwa na kiongozi wa chama cha Freedom Party, HEINZ CHRISTIAN STRACHE, imekubaliwa na mahakama.

Chama hicho kiliwasilisha hoja ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo kikidai kuwa ulijaa dosari wakati wa kuhesabu kura za watu ambao hawakuwa kwenye vituo vya kupigia kura.

Mahakama imeitisha marudio ya uchaguzi huo, ambao unatarajiwa kufanyika kati ya mwezi Septemba na Oktoba, na ambao huenda ukapelekea chama cha siasa za mrengo wa kulia, kuliongoza taifa hilo mwanachama wa Umoja wa laya kwa mara ya kwanza.

XS
SM
MD
LG