Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 11:41

Uchaguzi wa Rais: Zoezi la kupiga kura lakamilika Ufilipino


Uchaguzi Ufilipino/ Ferdinand "Bongbong" Marcos Jr.

Mtu anayetarajiwa kushinda katika uchaguzi huo ni Ferdinand Bongbong Marcos Jr, mtoto wa kiume wa diktekta wa zamani wa taifa hilo.

Kura za maoni zimeonyesha kuwa anaweza kupata ushindi mkubwa ikimaanisha kwamba ukoo wa Marcos uliopinduliwa na uasi wa watu miaka 36 iliyopita unaweza kutwaa tena madaraka.

Mpinzani wake mkuu ni Leni Robredo mliberali ambaye alimshinda kwa taabu bwana Marcos katika kinyang’anyiro cha makamu wa rais mwaka 2016.

Lakini wakusanyaji wa kura ya maoni katika kampeni hii wameonyesha mara kwa mara mrithi wa Marcos yuko mbele kwa asilimia 30.

Ilitarajiwa watu wengi watajitokeza katika taifa hilo lenye watu wanaostahili kupiga kura milioni 67.5 huku wengi wakiwa wamejipanga majira ya alfajiri Jumatatu kupiga kura zao kwenye vituo katika shule na vituo mbalimbali.

Raia wa Ufilipino wanapiga kura za rais, makamu wake, maseneta, wabunge na maelfu ya maafisa wa ngazi za chini kote katika visiwa hivyo takriban 7,600.

XS
SM
MD
LG