Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, serikali inalaumu Esther Lynch ambaye ni katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi vya Ulaya kutoka Ireland kwamba ameingilia masuala ya ndani ya Tunisia wakati wa maandamano ya Jumamosi kwenye mji wa Sfax, yakilalamikia utawala wa Saied.
Muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini humo UGTT, uliitisha maandamano ya kitaifa kupinga msako unaofanywa na serikali dhidi ya wapinzani wa kisiasa, wanahabari, majaji, wafanyabiashara pamoja na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
Wakati akihutubia waandamanaji. Lynch aliitisha kuachiliwa kwa kiongozi wa wafanyakazi Anis Kaabi aliyekamatwa na maafisa wa usalama mwezi uliopita. Aliomba serikali kushauriana na uongozi wa UGGT, pamoja na kuimarisha uchumi ambao unaelekeza taifa hilo kufilisika. Mzozo wa kisiasa umeendelea kuongezeka baada ya uchaguzi wa bunge mwezi uliopita, uliovutia asilimia 11 pekee ya walipigakura.
Facebook Forum