Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, chanzo cha mlipuko huo hakijabainishwa, wakati baadhi ya vyombo vya habari vya ndani vikiripoti kwamba majengo kadhaa yaliporomoka.
Mlipuko huo unaripotiwa kusikika kwenye mji mkuu wa jimbo la Oyo wa Ibadan, uliyoko umbali wa kilomita 130 kutoka kwenye mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria wa Lagos.
Awali mkuu wa mawasiliamo wa jimbo hilo Prince Dotun Oyelade alisema kwamba wakazi wa Ibadan pamoja na vitongoji vyake, walisikia mlipuko usio wa kawaida, mida ya saa 2 za usiku. Serikali ya jimbo imeomba wakazi kuwa watulivu, wakati ikiendelea kushugulikia mkasa huo.
Forum