Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:56

Tiger Woods aachana na mkewe Elin


Tiger Woods bingwa wa dunia wa mchezo wa Golf na mke wake mzaliwa Sweden Elin Nordegren wametangaza kwamba wanaachana na wanasikitika kutokana na hali hiyo.

Hayo yalitangazwa kwenye taarifa ya pamoja iliyotolewa na mawakili wao wakisema "tumesikitika kwamba ndoa yetu imefikia kikomo na tunatakiana kila la heri katika maisha yetu ya baadae. Ingawa tumeachana, lakini sisi ni wazazi wa watoto wetu wawili wazuri na furaha yao imekua na daima itakua jambo muhimu kabisa kwetu sote wawili".

Maelezo zaidi juu ya makubaliano ya talaka haijatangazwa, lakini wote watashirikiana katika ulezi wa watoto wao.

Woods na Nordegren waliowana Barbados Oktoba 2004, katika kile kilicho chukuliwa kua ndoa ya ndoto kama ilivyopangwa kwenye kitabu cha riwaya hadi pake kashfa ya ngono kuifikisha tamati. Wana watoto wawili, binti mwenye umri wa miaka mitatu na mtoto wa kiume mwenye umri wa mwaka moja.

XS
SM
MD
LG