Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 10, 2026 Local time: 14:56

Thailand kufufua mpango wa mwanamke kushika mimba kwa niaba ya watu fulani

Ni miongoni mwa mpango wa  mageuzi yenye lengo la kubadili kiwango cha uzazi kinachopungua huko Thailand

Mipango ya Thailand ya kufufua tena biashara yake kwa mwanamke kukubali kushika mimba na kujifungua mtoto kwa niaba ya familia fulani maarufu kama SURROGACY baada ya zoezi hilo kupigwa marufuku karibu muongo mmoja uliopita baada ya mfululizo wa kashfa, inafufua tena hofu ya zamani kuhusu usafirishaji wa binadamu wa watoto na wanawake walioajiriwa kushika mimba hizo.

Kuna wasiwasi mwingi, alisema Sunwanee Dolah, ambaye anatoa ushauri kwa makundi ya ndani kuhusu biashara ya binadamu na masuala ya haki za wanawake. Labda watu wengi watakuwa waathirika wa biashara ya usafirishaji binadamu, au watalazimika kutoa huduma hiyo kama biashara ya SURROGACY, itahalalishwa, aliiambia VOA.

Sura Visetsak, ambaye anaongoza idara inayotoa msaada wa huduma za afya katika Wizara ya Afya ya Umma, alitangaza mipango hiyo mapema mwezi huu kwa rasimu ya sheria ya kuhalalisha biashara ya “Surrogacy” kwa wanandoa wa ndani na wa kigeni, kuwa miongoni mwa mpango wa mageuzi yenye lengo la kubadili kiwango cha uzazi kinachopungua nchini humo.

This item is part of

Forum

XS
SM
MD
LG