Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 00:48

Sudan yashutumiwa kutumia silaha za sumu Darfur.


Mwamamke mmoja akiwa na mwanae katika kambi ya wakimbizi ya Zam zam kaskazini mwa Darfur Sudan.

Tangu mwezi Januari watu katika eneo la Jebel marra huko Darfur wameripoti kupata malenge lenge na upele kwenye ngozi zao, wakiwa na matatizo ya ngozi kuchubuka, matatizo ya macho ikiwemo kupoteza nguvu ya kuona, kutapika damu, kuharisha na matatizo makubwa ya kupumua.

Zote hizi ni dalili za kuvuta hewa ya kemikali shirika la Amnesty International linasema kuwa inatoka kwenye silaha ambazo serikali ya Sudan ilizitumia.

Takriban watu 250, wakiwemo watoto wengi, huenda wamefariki dunia ikiwa ni matokeo ya mashambulizi ya kemikali, na mamia zaidi wamejeruhiwa, linasema kundi hilo la kutetea haki.

Ripoti iliyotolewa na Amnesty alhamisi imeelezea kwamba majeshi ya usalama ya Sudan kwa makusudi yamewalenga raia na mali zao, ikiwemo kutumia kemikali ambayo imepigwa marufuku, na imetumiwa katika kiasi cha vijiji 32 huko Jebel marra.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG