Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:50

Sudan Kusini yailaumu Kenya kumpokea Machar


Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar (R) na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wakibadilishana mkataba wa amani huko Addis Ababa, Ethiopia, Mei 9, 2014.
Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini Riek Machar (R) na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir wakibadilishana mkataba wa amani huko Addis Ababa, Ethiopia, Mei 9, 2014.
Sudan Kusini inadai kwamba Sudan inajaribu kuhujumu uhalali wa serikali ya Rais Salva Kiir na uhusiano kati ya mataifa hayo mawili baada ya wawakilishi wa waasi wanaomtii Makamu Rais wa zamani Riek Machar waliporuhusiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari katika nchi hiyo jirani mwishoni mwa wiki.

Msemaji wa rais wa Sudan kusini Ateny Wek Ateny pia alitoa lawama kama hizo kwa Kenya kwa kumpa Machar mapokezi yenye hadhi ya kiongozi ya zulia jekundu kufuatia mkutano wake wa hivi karibuni na Rais Uhuru Kenyatta kama juhudi za Nairobi za kutatua mzozo wa Sudan Kusini.

Amesema “Kwa serikali ya Kenya kumpokea kiongozi wa waasi kwa heshima za zulia jekundu ni tusi kwa uhuru wa Sudan Kusini. Upinzani haupokelewi kwa zulia jekundu wakati wanapotembelea nchi za nje, alisema Ateny”.

Aliongeza kusema “kama Raila Odinga, Makamu Rais wa zamani wa Kenya anakuja Sudan Kusini hatuwezi kumwekea zulia jekundu, kwa nini Kenya wanafanya hivyo? Kwa sisi ni kuitusi Jamhuri ya Sudan Kusini”.

“Kama Rais wa Kenya alikuwa mwenyeji wa kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini kwa misingi kwamba alikuwa Makamu Rais wa zamani, basi ingefaa William Rutto- Makam Rais wa Kenya angetakiwa kufanya hivyo, alisema Ateny.

“Hili ni jaribio la kuhujumu uhalali wa serikali ya Juba,” alisema Ateny.Matamshi ya Ateny yalifuatia mkutano wa wajumbe wa waasi na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum. Ujumbe ulikuwepo Sudan kama sehemu ya maandalizi ya ziara ijayo ya Riek Machar huko Sudan.
XS
SM
MD
LG