Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 19:51

Shule zafunguliwa Pakistan


Mwanafunzi akisindikizwa kwenda shule na mzazi wake Jumatatu, Desemba 12, 2005 baada ya shule ya kijeshi iliyoshambuliwa mwaka jana kufunguliwa tena.

Shule zimefunguliwa tena Jumatatu kote nchini Pakistan, ikikaribia mwezi mmoja toka wanamgambo wa Taliban waliposhambulia na kuwauwa watoto 134 na wafanyakazi 16 katika shule mjini Peshawar.

Mkuu wa jeshi la Pakistan, Generali Raheel Sharif, aliwakaribisha binafsi wanafunzi waliorudi shuleni mapema leo katika shule ya umma inayosimamiwa na jeshi, ambako kulifanyika mauaji siku ya Desemba 16, mwaka jana.

Maafisa wa Pakistan wametoa mwito kwa shule zote nchini humo kuongeza ulinzi zaidi ili kutoruhusu mashambulizi zaidi.

Shule hiyo ya umma inayosimamiwa na jeshi imejenga ukuta mrefu, kuweka waya wa ulinzi pamoja na camera za video kuzunguka eneo hilo ikiwa ni hatua ya kutoruhusu mashambulizi baadae.

Hata hivyo maofisa hawakuruhusu baadhi ya shule kufunguliwa Jumatatu kutokana na kutokuwepo kwa juhudi madhubuti za ulinzi.

XS
SM
MD
LG