Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 19:34

Shirika la Human Rights Watch lawashutumu wanajeshi wa Cameroon kwa "mauaji"


Wanajeshi wakishusha bendera ya Cameroon
Wanajeshi wakishusha bendera ya Cameroon

Shirika la kutetea haki  la Human Rights Watch limewashutumu wanajeshi wa Cameroon kwa "mauaji", "kuzuiliwa kiholela" na "uporaji" wa vijiji na vituo vya afya katika eneo la Kaskazini-Magharibi.

Ripoti ya shirika hilo iliwashutumu wanajeshi wa serikali kwa kuwaua takriban watu 10 na kutekeleza unyanyasaji mwingine kati ya Aprili 24 na Juni 12 mwaka huu, wakati wa operesheni za silaha dhidi ya wanaotaka kujitenga katika eneo hilo linalozungumza luhgha ya Kiingereza.

Wanajeshi hao pia wameripotiwa kuteketeza nyumba 12, kuharibu na kupora vituo vya afya, kuwaweka kizuizini kiholela watu 26, na inakisiwa kuwa idadi ya waliotoweka imefikia 17.

Tangu mwaka 2016, wanajeshi wa Cameroon wamekuwa wakishirikisha vikundi mbalimbali vya watu wanaotaka kujitenga wanaoendesha vita vya msituni katika maeneo yenye watu wengi wanaozungumza Kingereza huko Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi kwa nia ya kuanzisha taifa lililojitenga la "Ambazonia".

XS
SM
MD
LG