Shambulio la ndege zisizo na rubani siku ya Jumatatu lililenga kambi ya jeshi kaskazini mwa Iraq inayotumiwa na vikosi vya Marekani na muungano wa kupambana na dhidi ya jihadi, maafisa wa Marekani na Iraq wamesema, katika tukio la hivi karibuni la aina hiyo.
Idadi ya mashambulizi yanayolenga muungano huo, ambao ulipeleka wanajeshi nchini Iraq kupambana na kundi la Islamic State, yameongezeka tangu kuanza kwa vita vya Israel na Hamas hapo Oktoba 7.
Katika tukio la Jumatatu, ndege isiyokuwa na rubani ilirushwa kuelekea kambi karibu na uwanja wa ndege wa Irbil, katika eneo la Kurdistan nchini Iraq, Yehia Rasool, msemaji wa Waziri Mkuu wa Iraq anayehusika na masuala ya kijeshi, amesema katika taarifa. Shambulio hilo lilisababisha majeruhi, Rasool alisema, bila kutoa maelezo zaidi.
Afisa wa jeshi la Marekani, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, aliithibitishia shirika la habari la AFP kwamba shambulio la ndege zisizokuwa na rubani lilirushwa “kwa vikosi vya Marekani na muungano” kwenye kambi ya jeshi la anga, na kuongeza kuwa “bado tunasubiri tathmini ya majeruhi na uharibifu wowote kama upo.
Forum