Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 06:53

Serikali ya Cameroon imeanza mchakato wa mazungumzo na upinzani nchini humo


ramani ya Cameroon na majimbo yake
ramani ya Cameroon na majimbo yake

Canada inakaribisha makubaliano ya pande husika nchini Cameroon kuingia katika mchakato wa kufikia suluhisho kamili la amani na kisiasa la mzozo huo waziri wa mambo ya nje M Mélanie Joly alisema katika taarifa siku ya Ijumaa

Serikali ya Cameroon na baadhi ya makundi yanayotaka kujitenga katika mikoa inayozungumza Kiingereza nchini humo wamekubaliana kuanza mchakato unaolenga kutatua mzozo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000, wizara ya mambo ya nje ya Canada imesema.

"Canada inakaribisha makubaliano ya pande husika kuingia katika mchakato wa kufikia suluhisho kamili, la amani na kisiasa la mzozo huo," waziri wa mambo ya nje M Mélanie Joly, alisema katika taarifa siku ya Ijumaa.

Taarifa hiyo ilisema Canada imekubali mamlaka ya kufanikisha mchakato huo na pande zote zimekubaliana kuunda kamati ya kiufundi kuanza kazi ya kuandaa hatua za kujenga imani.

Mzozo huo wa kivita, ulioanza mwaka 2017, unatokana na kutengwa kwa jamii inayozungumza Kiingereza nchini Cameroon na walio wengi wanaozungumza Kifaransa katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Tangu wakati huo, makundi ya wanamgambo wanaotaka kujitenga yamekuwa yakipambana na wanajeshi wa serikali katika mikoa miwili inayozungumza Kiingereza katika jaribio la kuunda taifa lililojitenga linaloitwa Ambazonia.

Mjadala wa kitaifa wa mwaka 2019 ambao ulitoa hadhi maalum kwa mikoa miwili ya inayozungumza kiingereza ulishindwa kutatua mzozo huo ambao umeongezeka. Takriban watu 800,000 wamekoseshwa makaazi, na watoto 600,000 hawana fursa kamili kwa elimu, Canada imesema.

XS
SM
MD
LG