Senegal ilijiandaa kwa siku ya pili ya machafuko leo Ijumaa baada ya hukumu ya kifungo kwa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko na kupelekea kuwa moja ya siku mbaya sana ya ghasia katika kumbukumbu za hivi karibuni.
Watu tisa waliuwawa katika makabiliano kati ya polisi wa kutuliza ghasia na wafuasi wa Sonko siku ya Alhamisi baada ya mgombea huyo wa urais kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili kwa ufisadi wa vijana uamuzi ambao unatia dosari nafasi yake ya kuwania urais mwaka ujao na upinzani unasema kuwa kuna ushawishi wa kisiasa.
Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop, katika mji mkuu wa Dakar, kimekuwa kitovu cha ghasia, huku waandamanaji wakichoma mabasi na kuwarushia mawe polisi wa kutuliza ghasia, ambao walijibu kwa kurusha mabomu ya kutoa machozi.
Mapema siku ya Ijumaa, vikosi vya usalama vilishika doria katika mitaa tulivu ya Dakar, ambayo ilikuwa imetapakaa matairi yaliyochomwa moto, mawe na vioo vilivyovunjika na kukiwa na makazi na biashara zilizoharibika. Makundi makubwa ya wanafunzi yalitolewa nje ya chuo kikuu wakiwa na vitu vyao.
Forum