Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 07:56

Reuters: Vyombo vya usalama vyahusika na uhalifu Darfur


Walinda amani huko Darfur wanaounda kikosi kijulikanacho kama UNAMID
Walinda amani huko Darfur wanaounda kikosi kijulikanacho kama UNAMID

Polisi na majeshi ya usalama nchini Sudan yamewapiga risasi na kuwaua pamoja na kuwateka raia huko Darfur mahala ambako hali ya kutokhofia kushtakiwa imekithiri. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Umoja wa Mataifa ulisema katika ripoti yake ya Ijumaa.

Ripoti hiyo ambayo pia iliorodhesha uhalifu uliotendwa na waasi hapo mwaka jana. Jeshi lilielezewa kufanya mashambulizi ya mambomu kwa njia ya anga na mashambulizi ya ardhini kwa raia pamoja na kuchoma moto vijiji katika kampeni ya kumaliza uasi huko Darfur kaskazini na kusini mwaka 2014.

Kikosi cha pamoja cha amani huko Darfur-UNAMID
Kikosi cha pamoja cha amani huko Darfur-UNAMID

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu ilisema kumekuwepo na ukiukaji mkubwa wa sharia za kimataifa. Walinzi wa amani wa Umoja wa Afrika-AU na Umoja wa Mataifa-UN ambao wanaunda kikosi cha pamoja huko Darfur wanaojulikana kama UNAMID walielezea kesi 411 za manyanyaso yaliyofanywa na pande zote katika mzozo.

XS
SM
MD
LG