Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:18

Republican watadhibiti mabaraza yote ya bunge Marekani


Seneta Rand Paul (L) na Seneta Mitch McConnell wote wa-Republican wakifurahia ushindi wa Novemba 4, 2014
Seneta Rand Paul (L) na Seneta Mitch McConnell wote wa-Republican wakifurahia ushindi wa Novemba 4, 2014

Chama cha Republican nchini Marekani kilipata udhibiti wa baraza la Senate katika uchaguzi wa awamu ya kati uliofanyika Jumanne. Chama hicho cha upinzani pia kinategemewea kupanua idadi ya wabunge wake katika baraza la wawakilishi ambalo tayari linadhibiti.

Ushindi wa chama cha Republican katika majimbo ya Arkansas, Colorado, Iowa , Montana, North Carolina, South Dakota na West Virginia, utabadili mizani ya madaraka jijini Washington.

Kiongozi wa walio wachache katika baraza la Senate Mitch McConnell alipambana vikali dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Democrat Alison Lundergan Grimes katika jimbo la Kentucky. Baadaye Jumanne jioni Grimes aliwashukuru wafuasi wake huku akitoa hotuba ya kukubali kushindwa.

Mitch McConnell
Mitch McConnell

McConnell alianza kupata uungaji mkono wa wengi katika siku za mwisho mwisho za kampeni na kushinda uchaguzi huo kwa muhula wa sita baada ya mpambano mkali dhidi ya mpinzani wake. Aliwaambia wafuasi wake kuwa uchaguzi huo haukumhusu yeye binafsi wala mpinzani wake. Alitupia lawama kali kwa serikali ya Rais Obama akisema imeshindwea kutoa huduma za kimsingi kwa wa-Marekani.

Rais Barack Obama hakugombania kiti chochote lakini wa-Republican wengi walitumia sera zake pamoja na mfumo wa bima ya afya kufanya kampeni zao wakisema mamilioni ya wa-Marekani hawana bima. Wengine walilenga sera za bwana Obama za nishati, uhamiaji na namna serikali yake inavyolishughulikia tatizo la Ebola na vitisho vya wanamgambo wa Islamic State huko Syria na Iraq.

Lakini kwa sasa macho yote yataelekezwa Washington huku bunge jipya likiapishwa mwezi Januari. Baadhi ya wa-Republican wanasema huku mabaraza yote mawili ya bunge yakiwa na wingi wa wabunge watafanya jitihada za pamoja kuifuta sheria ya mfumo wa bima ya afya maarufu kama Obamacare na kumpa changamoto kali bwana Obama juu ya swala la uhamiaji na mengine.

XS
SM
MD
LG