Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 04:37

Rais wa Zimbabwe atoa wito kwa bara la Afrika


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe

Wakati akikabidhi wadhifa unaozunguka wa mwenyekiti wa umoja wa Afrika, rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alisema Afrika itajitowa kwenye Umoja wa mataifa, katika siku za usoni .

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe pamoja na baadhi ya raia, walilaani wito wa rais Mugabe kutaka bara la Afrika lijitowe katika umoja wa mataifa.

Mwishoni mwa wiki rais huyo mwenye umri wa miaka 91 alisema iwapo bara hilo halitopewa nafasi moja kama mwanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja mataifa, basi wanachama wa AU wajitowe katika bodi hilo.

Wakati akikabidhi wadhifa unaozunguka wa mwenyekiti wa umoja wa Afrika, rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alisema Afrika itajitowa kwenye Umoja wa mataifa, katika siku za usoni , iwapo hakutakuwa na mabadiliko katika baraza la usalama la umoja mataifa, ambalo halina mwanachama wa kudumu kutoka bara la Afrika.

Mugabe alielekeza matamshi yake kwa katibu mkuu wa umoja mataiba Ban Ki Moon, ambaye alikuwa akihudhuria mkutano wa umoja wa Afrika huko Ethiopia.

“Tutapigania utambulisho wetu wenyewe, kwa hadhi yetu kama waafrika. Wengine ni wanachama wa kweli wa baraza hilo, lakini sisi ni wanachama bandia. Hatuwezi kuendelea kuwa wanachama bandia. Vipi watu kidogo wanalitawala baraza la usalama la umoja wa mataifa. Ni nchi za ulaya na America pekee yake. Iwapo umoja wa mataifa unataka kudumu, basi lazima bara la Afrika nalo pia liwe mwanachama sawa wa baraza hilo.”

Bw Mugabe, aliendelea kutaja China, kuwa nayo pia ni mwanachama wa kudumu katika baraza hilo. Wengine ni Russia, Marekani, Uingereza na Ufaransa.

Katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani cha Zimbabwe, Movement for Democratic Change, Bw. Douglas Mwonzora, alisema taifa lao linakabiliwa na masuala mengine tete Zaidi kuliko yale ambayo Bw. Mugabe analenga.

Kabla ya mkutano wa umoja wa Afrika kufanyika huko Ethiopia, Mugabe na rais wa Equitorial Guinea, Teodoro Obiang, walisema kuna haja ya mabadiliko katika baraza la usalama la umoja mataifa, ambalo linapaswa kuwa na angalu nafasi mbili za kudumu zilotengwa kwa ajili ya bara la Afrika, katika baraza la usalama la umoja wa Mataifa.

Kujitowa katika umoja mataifa kutamaanisha kwamba Zimbabwe, ambayo sekta zake za kijamii kama vile afya na elimu, zinategemea sana idara za bodi hilo kama vile WFP, UNICEF, WHO na UNFPA, na Zimbabwe itapoteza mengi. Hilo huenda likakabiliwa vilevile na nchi nyengine zenya chumi dhaifu.

XS
SM
MD
LG