Matamshi hayo aliyatoa kwenye kanisa moja la kiinjilisti jimboni Florida hapa Marekani na ndiyo ya kwanza mbele ya umma kuhusu azma yake ya kurejea nyumbani.
Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali wa kulia amekuwa hapa Marekani katika mji wa Olrando tangu Desemba 31, siku moja kabla ya kuapishwa kwa mshindani wake mwenye msimamo wa mrengo wa kushoto Luiz Inacio da Silva kuwa rais wa Brazil.
Hafla ya Jumamosi kwenye kanisa hilo iliendeshwa kwa lugha ya kireno, kwa ajili ya wafuasi wake wanaoishi hapa Marekani na iliandaliwa na kundi la Yes Brazil USA. Waliohudhuria walimshangilia kiongozi huyo muda wote wa hafla hiyo.
Kumekuwepo na mjadala katika wiki za karibuni kuhusu kurejea kwake nchini Brazil ambako anakabiliwa na uchunguzi kutokana na tuhuma za matumizi mbaya wa madaraka.
Facebook Forum