Weckremesinghe alikuwa katika ziara yake ya kwanza nchini India tangu achukue madaraka mwaka mmoja uliopita, baada ya mgogoro wa uchumi uliolikumba taifa lake, na kupelekea kujiuzulu kwa mtangulizi wake.
Kiongozi huyo ameizuru India wakati mataifa yote mawili yakijitahidi kufufua ushirikiano ulioathiriwa na ushawishi wa China, hasa kwenye taifa lake ambalo ni kisiwa kilichoko baharini kusini mwa India.
Kabla ya kuporomoka kwa uchumi wa Sri Lanka, China ilikuwa imewekeza mabilioni ya dola kweye miradi ya miundombinu ambayo ilizua hofu za kiusalama kwa India. Ushirikiano kati ya Colombo na New Delhi hata hivyo ulifungua ukurasa mpya baada ya India kutoa msaada wa dola bilioni 4 za kulisaidia taifa hilo lililotatizika.
Forum