Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 22, 2025 Local time: 20:53

Rais wa Mauritania anaisihi Mali kujiunga tena na kikosi cha Sahel cha G5


Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani wakati wa mkutano wa G5 Sahel mjini Nouakchott, Mauritania. June 30, 2020.
Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani wakati wa mkutano wa G5 Sahel mjini Nouakchott, Mauritania. June 30, 2020.

Rais wa Mauritania siku ya Jumatatu aliisihi Mali kujiunga tena na kikosi cha Afrika Magharibi kinachopambana dhidi ya wanamgambo wa kislamu kinachojulikana kama G5 Sahel ambalo ilijiondoa mwaka jana.

Mali ilitangaza uamuzi wake hapo Mei 2022 ikishutumu kupoteza uhuru na kujiimarisha ndani ya kikundi cha kikanda. Mwaka 2021, Chad ilikusudiwa kukabidhi urais wa G5 kwa Mali lakini haikufanya hivyo hatua ambayo Bamako iliitafsiri kama uingiliaji kati wa Ufaransa.

Natumai uondokaji huu utakuwa wa mfupi sana, Rais Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani alisema katika hotuba katika mji mkuu wa Nouakchott. Alisema uamuzi wa utawala wa kijeshi, Ufaransa kuondoa vikosi vyake vya mwisho kutoka Mali vilivyopelekwa chini ya kikosi chake cha kupambana na jihadi cha Barkhane, pamoja na mgogoro wa Sudan ni matukio ya kusikitisha.

Forum

XS
SM
MD
LG