Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:39

Rais wa Ghana adai kwamba Burkina Faso imewapa mamluki wa Russia haki ya kuchimba madini nchini mwao


Rais wa Ghana Nana Addo Akufo, aliyedai kuwa Burkina Faso imewapa mamluki haki za kuchimba madini.
Rais wa Ghana Nana Addo Akufo, aliyedai kuwa Burkina Faso imewapa mamluki haki za kuchimba madini.

Waziri wa madini wa Burkina Faso Jumanne amekanusha madai kutoka kwa rais wa Ghana Nana Akufo Addo kwamba taifa lake limewalipa mamluki wa Russia kwa kuwapa haki za kuchimba madini.

Akufo Addo wiki iliyopita alizua mtafaruku baada ya kudai kwamba Burkina Faso iliajiri mamluki kutoka kundi la Wagner la Russia, ili kusaidia kwenye mapambano dhidi ya wanamgambo wa kiislamu.

Wakati akizungumza na wanahabari akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Akufo Addo alisema kwamba anaamini mgodi uliyopo kusini mwa Burkina Faso umepewa mamluki hao kama njia ya malipo kwa huduma zao.

Serikali ya Burkina Faso haijakanusha wala kukubali madai hayo, ingawa imemuita balozi wa Ghana nchini humo kwa mkutano siku ya Ijumaa, ili afafanue zaidi kuhusu matamshi ya rais wake.

Mali ambayo ni jirani wa Burkina Faso, mwaka uliopita pia iliwakaribisha mamluki wa Wagner, ili kuwasaidia kwenye vita dhidi ya wanamgambo.

XS
SM
MD
LG