Rais Barack Obama amelihutubia taifa Jumatatu usiku akisisitiza kwamba jeshi la taifa litaendelea na kazi zake wakati baadhi ya shughuli za serikali kuu zinafungwa kuanzia Jumanne baada ya bunge kushindwa kukubaliana juu ya bajeti ya mwaka 2013 - 2014.
Baada ya wabunge wa Baraza la Wawakilishi kushindwa kukubaliana ilipofika saa sita usiku hapo Jumatau juu ya bajeti ya matumizi, serikali kuu ililazimika kutangaza kwamba baadhi ya idara kadhaa za serikali zitabidi kufungwa.
Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiendelea bungeni kuhusiana na sheria ya kihistoria ya Rais Obama ya kutoa huduma nafuu ya afya ambayo inafahamika sana kwa jina la "Obamacare".
Baraza la wawakilishi linalo-ongozwa na Warepublican liliidhinisha mswada wa matumizi ya serikali lakini kwa kuambatanisha kufutwa kwa sheria ya Obamacare. Na mara tatu Baraza la Seneti linalodhibitiwa na wademokrat limepinga mswada huo.
Kutokanana Bunge kutokubaliana juu ya kupitisha mswada wa kuongeza muda wa matumizi ya serikali kuu, sheria ya Marekani inahitaji idara zote ambazo hazina shughuli muhimu kufunga ofisi zake za kazi kuanzia Oktoba mosi, yaani siku ya Jumanne.