Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 10:24

Rais Obama na rais Putin wazungumzia Syria.


Rais wa Marekani Barack Obama alipokutana na rais wa Russia Vladimir Putin kandioni mwa mkutano wa G8.
Rais wa Marekani Barack Obama alipokutana na rais wa Russia Vladimir Putin kandioni mwa mkutano wa G8.
Rais wa Russia Vladmir Putin anasema Marekani na Russia zina mtazamo tofauti juu ya Syria lakini wanakubaliana kwamba ghasia lazima zisimamishwe na pande zote na kushauriana juu ya suluhisho.

Bw.Putin na Rais wa Marekani Barack Obama walizungumza juu ya Syria Jumatatu pembeni ya mkutano wa G8 huko Ireland Kaskazini.

Bw.Obama alimshukuru rais wa Russia kwa kile alichokiita mazungumzo mazuri. Alikubali kwamba mtazamo wao juu ya Syria hauingiliani. Lakini alisema pande zote zina mtazamo unaofanana wa wa kuzuia ghasia na matumizi ya silaha za kemikali.
XS
SM
MD
LG