Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:23

Rais Biden anamkaribisha Waziri Mkuu wa Japan huko White House


Rais wa Marekani Joe Biden (L) akiwa na Waziri Mkuu wa Japan Kishida Fumio(Foto: Zhang Xiaoyu via REUTERS)
Rais wa Marekani Joe Biden (L) akiwa na Waziri Mkuu wa Japan Kishida Fumio(Foto: Zhang Xiaoyu via REUTERS)

Kabla ya mkutano wa Biden na Fumio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin pamoja na wenzao Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Hayashi Yoshimasa na Waziri wa Ulinzi Hamada Yasukazu walifanya mabadiliko kadhaa katika eneo la ulinzi

Rais wa Marekani Joe Biden anamkaribisha Waziri Mkuu wa Japan Kishida Fumio huko White House siku ya Ijumaa katika ziara ambayo inasisitiza kuongezeka kwa muungano wa kimkakati kati ya Marekani na Japan na hisia zinazoongezeka za Tokyo za hatari huku kukiwa na vitisho vya usalama wa kikanda, hasa kutoka China, na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Kabla ya mkutano wa Biden na Fumio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin pamoja na wenzao wa Japani Waziri wa Mambo ya Nje Hayashi Yoshimasa na Waziri wa Ulinzi Hamada Yasukazu walifanya mabadiliko kadhaa katika eneo la ulinzi, mipango ya mafunzo ya kijeshi na uhusiano wa komandi ikiwa ni pamoja na mipango ya kupanga upya vitengo vya Jeshi la Wanamaji la Marekani vilivyopo Okinawa.

Mabadiliko hayo yaliyotangazwa mjini Washington siku ya Jumatano yanaashiria washirika hao wawili wanachukulia kwa uzito zaidi uwezekano wa vita katika eneo la Indo-Pasifiki iwapo kutatokea shambulio la China dhidi ya Taiwan au mashambulizi ya nyuklia ya Korea Kaskazini.

Inaweka nguvu Mkakati mpya wa Usalama wa Taifa wa Japani uliotolewa hapo Desemba hiyo inaonya juu ya uwezekano kwamba "hali mbaya inaweza kutokea katika siku zijazo katika eneo la Indo-Pasifiki, haswa East Asia," na inatoa wito wa uwezo wa kukabiliana masafa marefu ambao utaiwezesha kufikia malengo katika China bara.

XS
SM
MD
LG