Lakini sababu ya kifo bado haijafahamika wazi.
Keita, anayejulikana pia kama IBK, aliongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kuanzia Septemba 2013 hadi Agosti 2020, kipindi cha misukosuko ambacho kilishuhudia uasi mkali wa Kiislamu ukichukua maeneo makubwa ya kaskazini na kati na kupelekea kupoteza umaarufu wake.
Alilazimishwa kutoka madarakani na mapinduzi ya kijeshi baada ya miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya serikali.
Mshauri wa zamani alisema alifariki akiwa nyumbani kwake katika mji mkuu Bamako.
Facebook Forum