Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba amekaidi hofu za wapigakura baada ya miaka kadhaa kuwa katika kivuli cha baba yake na kuzima uvumi wa kifo chake kutokana na kuwa katika hali mbaya ya kiafya akitangaza Jumapili kwamba atawania muhula wa tatu.
Bongo mwenye umri wa miaka 64, ambaye alipatwa na kiharusi miaka mitano iliyopita, amekuwa akizungumziwa kuhusu afya yake ikichochewa zaidi na kutoonekana kwake kwa umma au katika shughuli zinazotangazwa moja kwa moja.
Lakini changamoto ya muhula wa tatu imeweka mashaka kwa baadhi ya watu walio karibu na rais huyo aliyeingia madarakani mwaka 2009, akichukua madaraka kutoka kwa baba yake, Omar Bongo Ondimba, mtawala wa nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kwa miaka 41.
Bongo alipata umaarufu mkubwa kwa herufi za mwanzo za majina yake; ABO, Ali B. Alizaliwa na Josephine Kama, ambaye alishika ujauzito akiwa msichana mdogo katika mji wa Brazzaville nchini Congo, wakati ambapo nchi hiyo ilikuwa bado sehemu ya utawala wa kikoloni wa Ufaransa ulioporomoka kwa kasi.
Forum