Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:53

Raia wa Tunisia wanapiga kura ya wabunge Jumamosi


Baadhi ya wakaazi wa Tunisia wakifanya kampeni za kutetea demokrasia nchini humo
Baadhi ya wakaazi wa Tunisia wakifanya kampeni za kutetea demokrasia nchini humo

Zaidi ya muongo mmoja tangu mapinduzi maarufu nchini Tunisia yaliyomuondoa madarakani dikteta Zine El Abidine Ben Ali vyama vya upinzani vimehimiza kususia uchaguzi huo ambao wanasema ni sehemu ya mapinduzi dhidi ya demokrasia pekee iliyojitokeza kutokana na vuguvugu la mapinduzi ya kiarabu ya 2011

Raia wa Tunisia wanapiga kura Jumamosi kuchagua bunge ambalo kwa kiasi kikubwa limepokonywa madaraka yake, chini ya mfumo wa urais uliowekwa na mkuu wa nchi Kais Saied baada ya kunyakua madaraka mwaka 2021.

Zaidi ya muongo mmoja tangu mapinduzi maarufu nchini Tunisia yaliyomuondoa madarakani dikteta Zine El Abidine Ben Ali vyama vya upinzani vimehimiza kususia uchaguzi huo ambao wanasema ni sehemu ya "mapinduzi" dhidi ya demokrasia pekee iliyojitokeza kutokana na vuguvugu la mapinduzi ya kiarabu ya 2011.

Uchaguzi wa bunge jipya lenye viti 161 unajiri baada ya Rais Saied kulivunja bunge lililopita Julai 25 mwaka 2021 kufuatia miezi kadhaa ya mzozo wa kisiasa uliozidishwa na janga la virusi vya corona.

Baadaye alivunja bunge, ambalo kwa muda mrefu lilikuwa limetawaliwa na mpinzani wake chama cha Ennahdha kilichoongozwa na Waislamu.

Saied siku ya Jumatano alitetea uamuzi wake, akisema kwamba "watu wa Tunisia, popote nilipokwenda, wote walikuwa wakiomba kuvunja bunge".

XS
SM
MD
LG