Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:17

Raia wa Nigeria waeleza walivyokuwa wakitumia twitter wakati wa marufuku

Magazeti yanavyoonekana baada ya serikali ya Nigeria kutangaza kuondoa marufuku ya Twitter,
huko Abuja, Nigeria, Jan. 13, 2022.
Magazeti yanavyoonekana baada ya serikali ya Nigeria kutangaza kuondoa marufuku ya Twitter, huko Abuja, Nigeria, Jan. 13, 2022.

Raia wa Nigeria siku ya Alhamisi waliitikia kwa ahueni   na kutojali uamuzi wa serikali wa kuondoa marufuku ya mtandao wa Twitter nchini humo wakisema wengi katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika walikuwa wanaendelea kuingia kwenye twitter kupitia mitandao ya binafsi ya  (VPN).

Kwa mwanamitindo Kingsley Osine, uamuzi wa serikali wa kuondoa marufuku hayo umewarudishia Wanigeria sauti zao.

Haikuwazuia wengi wetu kutweet, lakini unajua tulikuwa tukitweet kwa hofu, lakini sasa tunaweza kutweet kwa uhuru, tunaweza kurusha sauti zetu kwa uhuru, alisema Osine.

Ikitangaza kumalizika kwa marufuku hiyo iliyodumu kwa miezi saba, serikali ya Nigeria ilisema Jumatano kampuni hiyo kubwa ya mtandao wa kijamii ya Marekani imekubali kufungua ofisi yake nchini Nigeria miongoni mwa masharti mengine yaliyowekwa na taifa hilo la Afrika Magharibi.

XS
SM
MD
LG