Takriban raia 34 wa kujitolea na wanajeshi sita walifariki katika shambulio linaloshukiwa kufanywa na wanajihadi huko kaskazini mwa Burkina Faso serikali ya mtaa katika eneo hilo ilisema Jumapili.
Kikosi cha wanajeshi na raia wa kujitolea walilengwa katika shambulio la watu wasiojulikana wenye silaha Jumamosi, muda wa saa kumi jioni kwa saa za huko karibu na kijiji cha Aorema gavana wa eneo hilo alisema katika taarifa akiongeza kuwa idadi ya awali ya vifo ilikuwa wasaidizi wa kujitolea 34 na wanajeshi sita.