Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 05:55

Putin adai Uchumi utaimarika


Rais wa Russia Vladmir Putin pichani
Rais wa Russia Vladmir Putin pichani

Pia Rais Putin, amedai kwamba sarafu ya rubo itaimarika tena baada ya kuanguka kwa kiwango kikubwa wiki hii.

Rais wa Russia, Vladimir Putin, amesema kwamba ana imani uchumi wa nchi hiyo utaimarika tena katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Pia Rais Putin, amedai kwamba sarafu ya rubo itaimarika tena baada ya kuanguka kwa kiwango kikubwa wiki hii.

Akiongea kwenye kikao cha kufunga mwaka na Wanahabari, amesema kwamba uchumi waweza kuimarika kwa haraka zaidi iwapo maswala kutoka nje yatabadilika.

Rais Putin, amesema kwamba akiba ya fedha inatosha kuimarisha hali ya uchumi.

Thamani ya sarafu ya rubo imeimarika alhamisi kabla ya hotuba ya Rais Putin.

Sarafu ya Russia ilianguka kwa kiwango kikubwa siku ya Jumanne, jambo ambalo lilisababisha Benki Kuu kuyapa uhakika mabenki na mashirika mengine ya fedha kuwa itaongeza mtaji kama ikihitajika.

Kwa wakati mmoja, sarafu ya rubo ilianguka na kufikia rubo 80 kwa dola moja ya Marekani.

Rubo imepoteza Zaidi ya asilimia 60 ya thamani yake dhidi ya sarafu kuu za Magharibi mwaka huu.

Russia imekumbwa na matatizo baada ya nchi za magharibi kuiwekea vikwazo kufuatia Rais Putin kujiingiza Crimea.

XS
SM
MD
LG