Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:15

Maoni yaonyesha Wakenya watapitisha katiba mpya


Katiba mpya Kenya inatazamiwa kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida.
Katiba mpya Kenya inatazamiwa kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida.

Utafiti wa maoni uliofanywa na mashirika mawili unaonyesha kuwa Wakenya watakubali katiba mpya katika kura ya maoni August 4.

Matokeo ya utafiti wa maoni yaliyofanya na mashirika mawili ya utafiti yanaonyesha kuwa endapo kura ya maoni ya katiba mpya ingepigwa leo hii Wakenya watapitisha katiba mpya kwa wingi.

Kulingana na matokea ya utafiti wa kampuni ya Synovate, siku 12 kabla ya kura ya maoni, asilimia 73 ya watu waliohojiwa wanasema watapiga kura ya "ndiyo" wakati asilimia 27 wanasema wataikataa katiba hiyo mpya.

Utafiti mwingine uliofanywa na kampuni ya Infotrack Harris unaonyesha kuwa asilimia 65 wataikubali katiba hiyo mpya na asilimia 25 wataikataa. Asilimia 10 bado hawajaamua watapiga upande gani, kulingana na utafiti wa Infotrack Harris.

XS
SM
MD
LG