Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 25, 2025 Local time: 09:17

Polisi huko Serbia wamefyatua gesi ya kutoa machozi kuwazuia wapinzani

Polisi wa Serbia wakiwazuia upinzani kuandamana katika jengo la halmashauri ya mji nchini humo.
Polisi wa Serbia wakiwazuia upinzani kuandamana katika jengo la halmashauri ya mji nchini humo.

Mamlaka za nchi hiyo zimekanusha wizi wa kura na kuelezea uchaguzi huo kujaza nafasi za wabunge na serikali ya mitaa kuwa wa  haki. Rais wa Serbia Aleksandar Vucic alisema Jumapili kwamba madai hayo ni uongo wa wazi uliochochewa na upinzani wa kisiasa.

Polisi nchini Serbia walifyatua gesi ya kutoa machozi kuwazuia mamia ya wafuasi wa upinzani kuingia katika jengo la halmashauri ya mji kwenye mji mkuu siku ya Jumapili wakipinga kile ambacho waangalizi wa uchaguzi walisema ni ukiukwaji mkubwa wa kura wakati wa uchaguzi mkuu mwishoni mwa juma lililopita.

Mamlaka za nchi hiyo zimekanusha wizi wa kura na kuelezea uchaguzi huo kujaza nafasi za wabunge na serikali ya mitaa kuwa wa haki. Rais wa Serbia Aleksandar Vucic alisema Jumapili kwamba madai hayo ni uongo wa wazi uliochochewa na upinzani wa kisiasa.

Rais wa Serbia Aleksandar Vucic akiwa katika mji mkuu Belgrade. Nov. 1, 2023.
Rais wa Serbia Aleksandar Vucic akiwa katika mji mkuu Belgrade. Nov. 1, 2023.

Vucic pia alidokeza kuwa ghasia hizo zilichochewa kutoka nje ya nchi. Akihutubia taifa wakati wa maandamano nje ya ukumbi wa mji wa Belgrade, aliwaita waandamanaji hao “wasaliti” ambao hawatafanikiwa kuiyumbisha serikali, na kusema “Haya sio mapinduzi”.

“Hawataweza kufanikiwa”, alisema Vucic. “Tunafanya kila tuwezalo kwa utulivu wetu na kwa upole kutowaumiza waandamanaji” ambao walikuja kwenye tukio hilo wakiandamana kwa amani.

Forum

XS
SM
MD
LG