Bayern na PSG wanapata shida kukwepana hivi karibuni wamekutana katika kampeni zao nne kati ya sita zilizopita, haswa wakati Bayern au Bavarians walipoifunga PSG katika fainali ya Ligi ya Mabingwa 2020.
Kikosi cha Julian Nagelsmann -Bayern kilishinda mechi zote sita za hatua ya makundi, lakini Paris walipita bila kushindwa pia. Ilikuwa ni magoli yalioweka tofauti kati ya timu hizi zilipokutana mara ya mwisho, katika robo fainali ya 2020/21, na pambano lingine hivi karibuni haliepukiki.
Katika mtanange mwingine Totenham Hotspur itakwaana na AC Milan kwenye uwanja wa Giussepe Meaza mjini Milan.
Facebook Forum